Saturday, April 20, 2013

Umoja wa wakristo wilayani Rungwe waandaa ibada ya kuombea amani taifa la Tanzania

Baada ya kutokea mauaji ya watoto wawili katika maeneo ya Busekelo wilayani Rungwe ,Umoja wa wakristo umeandaa ibada ya kuombea amani wilaya hiyo pamoja na taifa kwa ujumla,ibada iyo imeudhuliwa na viongozi mbalimbali wa  dini,kwa upande wa serikali uliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya rungwe

Friday, April 19, 2013

Japokuwa kunarasilimali za kutosha lakini wananchi wake bado wanakabiliwa naumasikini.....,

Richa ya kuwepo kwa rasilima za kutosha katika wilaya ya Rungwe kama vile vivutio vingi vya utalii na aridhi nzuri ya kilimo ,lakini wananchi wa wilaya hii wanakabiliwa na umasikini.hii  ni kwa sababu na wakazi wengi kutozitumia rasilima hizo,Pili ni uzembe wa viongozi kuto kuwaamasisha wanchi katika shughuli za maendeleo,kwa mfano sekta ya utalii tu wilayani rungwe kama itapata furusa ya kutangazwa basi itachangia kwa kiasi kikubwa sana ustawi wa wilaya hii pamoja na taifa kwa ujumla.

Friday, April 12, 2013

Wazazi shule ya sekondari Bujinga wilayani Rungwe walalamikia uongozi wa shule hiyo.

Wazazi shule ya sekondari Bujinga wilayani Rungwe  wamemwomba mkuu wa wilaya hiyo ajaribu kuutanzama uongozi wa shule hiyo kwa makini,hili  kutatua kero zinazosababisha wanafunzi kuendelea kufeli.

Monday, April 1, 2013

Kama tutaiangalia kwa jicho la tatu wilaya ya rungwe,tatizo la umeme nchini Tanzania litakuwa limekwisha

Tatizo la umeme linalotusumbua nchini Tanzania linawezakuisha endapo tutaweza kuzitumia rasilimali za Rungwe vizuri basi  tatizo la umeme litakuwa historia nchini kwetu, rungwe kuna vyanzo vya umeme kama vile makaa ya mawe kiwila,mapolomoko ya maji mbalimbali yanayopatikana katika mlima rungwe kama kaparogwe falls.

Thursday, March 28, 2013

Rungwe ni bustani ya Adeni

Sababu inayonifanya  kusema rungwe ni bustani ya Adeni,  ni kuwepo kwa hali ya hewa nzuri  muda wote wa mwaka  na kingine ni kuwepo kwa bustani za asili zenye mimea ya kuvutia na wadudu na wanyama ambao awapatikani sehemu nyingine yoyote zaidi ya Rungwe....

Thursday, March 21, 2013

WANANCHI RUNGWE wamefurahishwa na kitendo cha mwekezaji kukubali kujenga kiwanda cha kusindika gesi inayochimbwa RUNGWE.

Wakazi wilayani Rungwe wamefurahishwa na kitendo cha mwekezaji kukubali kujenga kiwanda cha kusindika gesi inayochimbwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya.


Hata hivyo licha kiwanda hicho kujengwa Rungwe Serikali imesisitiza kuwa gesi hiyo ni mali ya watanzania wote na hakuna mwananchi wa Rungwe mwenye haki ya kuikatalia isisafirishwe kwenda maeneo mengine ya nchi.